Tengeneza application kwa kutumia Appy Pie!

Baada ya kutoa makala iliyoeleza namna ya kutengeneza application bila coding leo hii tunakuletea website au mtandao utakao kuwezesha kutengeneza application kiurahisi zaidi ndani ya mda kidogo!


Bila shaka kwa wengine Appy Pie yaweza kuwa geni akati kwa wengine si geni. Huu ni mtandao utakao kuwezesha kutengeneza application bila ya kuwa na ujuzi juu ya kuandikia code! Mtandao huu umekuwa ukitumiaka na watu mbalimbali na hii ni kutokana na kutoa application zenye ubora wa hali ya juu!

#UTENGENEZAJI_WA_APPLICATION.
Tafadhali fuata maelekezo yafuatayo ili uweze kufanikiwa katika utengenezaji wa application yako.

#Mahitaji
1. Barua pepe (Email) (hii ni lazima)
2. Password (lazima)
3. google account
4. Facebook account

#Hatua
1. Tembelea mtandao wa Appy Pie kwa kubofya HAPA.
2. Jisali

Waweza kutumia google account, Facebook account au ukajisajili upya.

3. Chagua jina la application na kitengo!
Chagua jina litakalo mvutia mtumiaji. Jitahidi liwe neno moja na yasizidi maneno mawili wala jina lisiwe lefu!

4. Bofya Skip
5. Chagua mwonekano wa application yako.
Hakikisha mwonekano wako unavutia na ni rafiki kwa mtumiaji.

6. Ongeza kurasa kadri ya ambavyo unavyotaka application yako iwe nazo.
usiweke kurasa zisizo kuwa na mhimu katika application na hakikisha mpangilio wake unakuwa ni mzuri.

7. Bofya save & continue

8. Chagua gharama za uendeshaji wa application. Kama hutaki kulipia basi chagua free (free application yako itakuwa na matangazo ya kampuni).
Sikushauli kuchagua "FREE". Chagua kulipia hata kile kimo cha chini kabisa.

9. Tiki kibox kisha Bofya Continue to my apps.
Subili utatumiwa link ya kudownload application yako ikiwa tayari.

#Mwisho
Kufikia hapo utakuwa umetengeneza tayari application yako na unawe ukaanza kupiga pesa kupitia application yako. Makala ijayo itahusu namna ya kuweka Application yako Katika masoko ya application za android(play store) na iphone.

Tafadhali washirikishe na wengine kupata elimu hii, pia tuandikie maoni yako hapo chini.




Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !