Tengeneza App za Android bila ya kuwa Na ujuzi wowote.

About us

Ulimwengu kwa sasa umekua sana kiasi kwamba karibia huduma zote unazipata kupitia simu yako ya mkononi, hii imesababisha watoa huduma wote ambao hutoa huduma mtandaoni kulazimika kutengeneza programu (App) kwaajili ya huduma zao, lakini katika kufanya hivyo bado unakutana na changamoto kwani ni lazima kuajiri watu kwaajili ya kufanya hivyo ndio mana leo Magoiga2016 tunakuletea maujanja ya kukuwezesha wewe mtu Wa kawaida kuweza kutengeneza application zinazo aweza kutumika katika Kifua cha Android, iTunes Na hata windows.




 Kumbuka hauitaji ujuzi mkubwa kufanya hivi bali unaitajika kuwa na kompyuta yenye uwezo wa kuunganisha internet pamoja na logo na picha mbalimbali za kuweka kwenye programu yako. Ni vyema kuangalia kwanza matumizi kisha ndipo ujue jinsi ya kutengeneza picha na logo za kuweka kwenye App au programu yako, pia ni vizuri kuwa na simu ya android kwaajili ya kutest programu yako kabla ujaamua kuipost kwenye masoko ya Android kama Play Store au Amazoni Store.

Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa ili kutengeneza programu hii ni vyema ukajua unataka kutengeneza programu ya aina gani zifuatazo ni tovuti 10 zitakazo kuwezesha kutengeneza programu mbalimbali kutokana na mahitaji yako.

10. Mobile Roadie
Kupitia Mobile Roadie Utaweza kutengeneza application bila ya kuwa Na ujuzi wowote juu ya utengenezaji Wa application ambapo mda mingine Inatakiwa kuwa umesoma.
Huu ni mtandao mmoja Wapo unaokupa nafasi ya kuweza kutengeneza application.

•Sifa za Mobile Rodie.

>Media
Katika swala zima la media hapa tunaongelea upande Wa Picha, video Na audio.
Kupitia mobile rodie Utaweza kupload media zako kirahisi Na unaweza kifanya setting zikawa zinajiweka zenyewe(automatically). Na swala la layout watumiaji wataweza kuona media zako zikiwa katika mpangilio mzuri Na Wa kueleweka (grid).

>Habari
Katika uwekaji Wa habari mbalimbali kupitia mobile roadie Utaweza kupost habari zako kiurahisi lakini pia unaweza kuweka habari automatically kupitia RSS feed.

>Matukio (events)
Kupitia Mobile Roadie utakuwa Na uwezo Wa kupost matukio mbalimbali yanaendelea au yanakutarajiwa kufanyika hapo baadae.

Mobile ina vipengele vingi ambavyo Utaweza kuvitumia kiurahisi bila bughudha.

09. Appmachine
 Huu pia ni mtandao mwingine unaotoa huduma ya kutengeneza Applications.

•Sifa za Appmachine

>Taarifa juu ya maendeleo ya application yako.
Kwa kutengeneza Application kupitia kwa huu mtandao Utaweza kupewa taarifa juu ya maendeleo ya application yako kwa kuangalia idadi ya watu wanakutumia Na idadi ya walio pakua application yako.

>Vitendea Kazi
Mtandao huu hutoa vitendea kazi vingi sana bure vitakavyo kidhi mahitaji yako pindi utakapo kuwa unatengeneza application yako.

>Uwezo Wa kutumika kabla ya kumalizika.
Najuana Wengi tumezoea kuitumia kitu ni mpaka kimalizike, lakini kwa kuitumia Appmachine Utaweza kuitumia Application yako kabla haijamalizika yaani hiki bado unaitengeneza Na unaitumia.


08. Andromo

Mtandao huu hukupa fursa ya kuweza kutengeneza application bila ujuzi pia

•Sifa za Andromo

>kukuwezesha kulink application yako mitandao ya kijamii

>kukuwezesha kuupakia mafile ya media mbalimbali

>Unakupa fursa ya kuchapa code zako mwnyw (HTML)

>unaweza ukaunganisha Na website yako.

07. Biznessapps

Kama Jina linavyo jieleza hii inawafaa sana kafanya biashara.

•Sifa za biznessapps

> Kumwezesha mteja kuweka order ya vitu vingi kwa wakati mmoja.

>Huduma kwa wateja.
Hapa hutoa mafunzo mbalimbali namba ya kuweza kutengeneza application bila ujuzi wowote kwa kutumia mtandao wao.

06.Buildfire

Hii moja kati ya mashirika yanayo milikiwa Na google.

•Sifa za build fire

>Maoni ya wateja
Kama ukitumia buildfire kutengeneza application bado utakuwa unauwezo Wa kupata maoni ya wateja kiurahisi

>uwekaji Wa media ni mrahisi sana

>Msaada
Pindi uatakapo kuwa unatengeneza application afu ukakwama unaweza kuomba msaada kutoka kwa kampuni.

>Lakini pia Utaweza kuunganisha mitandao ya kijamii zaidi yamoja.


05. Fliplet

Hii ni mahususi kwaajili ya kafanya biashara.

•Sifa za fliplet

>Hukupa uwezo Wa kuhifadhi data zako kwenye application

>uwezo Wa kuwa katika platform tatu yaani smartphone, tablet Na kompyuta.


04. ibuildapp
Mtandao huu pia hutoa fursa ya kukuwezesha wewe mwenye nia ya kumiliki application kuweza kufikia lengo lako

•Sifa za ibuildapp

>Platform
Hukupa fursa ya kutengeneza application itakayo weza kutumika katika platform mbili yaani Android and iOS

>Notification
Hukupa fursa ya kuwezesha notification katika application yako

>Advertisements
Hukupa fursa ya kuweza matangazo yako.

03. Appsgeyser

Hii inawafaa sana wale wanaopenda michezo ya chemsha bongo Na watengeneza magemu.

•Sifa sake

>search
Hii itakuwezesha kuweza kusearch bitu mbalimbali

>Messenger
Pia kuna sehemu maalumu cha kukuwezesha kutuma ujumbe wa maneno

>Lakini pia hukupa mifumo Na aina mbalimbali za aina za magemu

02. Appmakr

•Sifa zake
>Mtandao wako uko haraka sana

>inakupa fursa ya kuwashirikisha Na marafiki zako.

>Uwezo wa kuwatumia ujumbe wa maneno watumiaji wako


01. Appypie

Appypie in moja kati ya mtandao unaoongoza kwa kutumiwa Na watengenezaji Wengine wa application.
Mtandao huu kwa sasa ndo unaoongoza kwa kutumiwa zaidi ulimwenguni Na hii inatokan Na ubora wa bidhaa zao.

°Sifa za Appypie

>Ndani ya hatua tatu unakuwa Umemaliza kutengeneza application yako.

>Hutoa design ya layout nzuri Na zenyewe ubora wa halo ya juu.

>Huduma kwa wateja 24/7/365

>vitendea KAZI vingi sana Na rahisi kutumika maana vinaeleweka kiurahisi.

>Hutoa mafunzo Bure pale utakapo hitaji.

>Ukikwama watakusaifia Bure.

>Tovuti yako inaeleweka kwa kila mmoja.

>Urahisi wa kuweka Application yako kwenye masoko kama play store Na Amazon

Unaweza ukapakua baadhi ya application zilizotengenezwa kwa Appypie halo chini;

°Magoiga2016

°

Kwa Leo tunaishia hapo.

Kwa mwenye swali, ushauri au mada ya kiteknolojia ambayo angependa tuijadili usisite kutuandia kwenye sanduku la maoni hapo chini.
 
Kwa habari nyingine za teknolojia usisite kututembelea tena Magoiga2016.blogspot.com au unaweza kupakua Application yetu kwa kubofya HAPA

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !