Ifanye kompyuta yako ukiiwasha ikuite jina lako.


Unaonaje pale unapoingia nyumbani kwako, kazini, ofisi za umma au mahala popote kwa kukaribishwa huku ukitajwa jina lako. Ni jambo linalofurahisha na kusisimua sana.

Pengine Kompyuta yako unayoitumia nyumbani au kazini ungependa ifanye kazi hiyo kila unapoiwasha. Leo tunakupa maujanja ya kuifanya Kompyuta yako ukiiwasha ikukaribishe kwa kuita jina lako.

Ni njia rahisi sana ya kufanya hilo liwezekane. Baada ya wewe kupitia maelekezo tutakayo kuwekea hapa kompyuta yako itaweza kukukaribisha kwa namna ya kipekee kabisa.

Kufanikisha zoezi hilo fanya na ufuate maelekezo tunayokuwekea hapo chini.

1. Kwanza fungua ukurasa wa Notepad na kisha ukopi na kupaste maneno hayo ya chini

Dim speaks, speech

speaks=”Welcome to your PC, Username“

Set speech=CreateObject(“sapi.spvoice”)

speech.Speak speaks


Ukurasa wako wa Notepad baada ya kuufungua paste maneno tuliyokupa na uweke jina lako kwa kufuta username
2. Badilisha username na uweke jina litakalokaribishwa pindi Kompyuta ikiwaka.

3. Sevu faili lako kwa vbs. Yaani kama file lako umelipa jina la Teknokona, basi weka nukta kisha vbs
yaani liwe Teknokona.vbs

4. Baada ya hatua hiyo unatakiwa ulikopi faili lako na kulipeleka kwenye Startup. Hapo itategemea unatumia Windows gani ili kufika.

Zingatia haya, Kama unatumia Windows XP: Nenda C:\Documents and Settings\All Users\Start Menu\Programs\Startup



Kama unatumia Windows Vista/7/8/8.1/10:

Nenda C:\Users\ {User Name}\AppData\Roaming\Microsoft\Windows\Start Menu\Programs\Startup


Weka tiki sehemu iliyowekwa mshale ili kuona folder zilizojificha

kompyuta yako ukiiwasha ikuite jina lako: Muonekano baada ya kuweka tiki kwenye hidden items
Ukifanya hatua zote vizuri, zoezi lako litakuwa limekamilika kwa kukaribishwa kwenye Kompyuta yako kila inapowaka. Sauti ambayo itakuwa ikikukaribisha ni ya kiume.

Pengine wengine hawatajisikia raha kukaribishwa na sauti ya kiume. Kama ni hivyo basi tumia maneno haya ya chini ili uwe unakaribishwa na sauti ya kike.

Dim speaks, speech

speaks=”Welcome to your PC, I Love Free Software”

Set speech=CreateObject(“sapi.spvoice”)

Set speech.Voice = speech.GetVoices(“gender=female”).Item(0)

speech.Speak speaks

Kama umependa maujanja haya jaribu nawe kwenye Kompyuta yako ili uone unavyokaribishwa kama stelingi kwenye Movie. Bila shaka umefanikisha zoezi lako. Usisite kutupa maoni yako hapo chini

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !