Namna ya kutengeneza Na kumiliki blogu.



Blogu ni teknolojia mpya inayowezesha watu binafsi kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao wa tarakilishi. Blogu inaweza kuchukuliwa kama ni shajara pepe. Neno "blogu" ni tafsiri ya Kiswahili inayotokana na neno la kiingereza, "blog." Neno "blog" limetokana na neno jingine, "weblog." Kimsingi, blogu ni aina ya tovuti ambayo huandikwa mara kwa mara na kwa mpangilio wa mambo mapya kutokea ukurasa wa mbele kuendana na tarehe na mwezi.

         Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano, blogu za maandishi, blogu za mkononi, blogu za picha, blogu za sauti, na blogu za video. Na pia zipo za Bure Na nyingine za kulipia. Kwa hapa tutaangazia zile za Bure kutoka kwenye kampuni ya google (blogger).

Mara nyingi watu wengi tumekuwa Na hamu ya kumiliki blogu bila mafanikio Na hii inatokana Na kushindwa wapi pa kuanzia.

Kabla ya yote fahamu mambo au vitu muhimu unavyotakiwa kuvijua au kuwa navyo pale unapotaka kuanzisha blogu yako:

 1.Barua pepe ya Gmail (gmail email address)
 2. Internet connection.
 3. Kifaa (kompyuta au simu)
 4. Fahamu kwanza blogu yako itahusu nini  Na walengwa wako ni akina nani.
 5. Hakikisha una mahitaji yote utakayo hitaji.
 6. Chagua jina la blogu yako.(mfano. Magoiga2016.blogspot.com )


Baada ya kuwa umekamilisha hayo mambo hapo juu, sasa tunaingia katika kutengeneza blogu kupitia blogger(blogspot):

HATUA.

01. Kupitia kifaa chako ingia mtandao ni Na tafuta www.blogger.com

02. Ingia (Sign In) kwa kutumia Gmail Account Yako na Password yako..hizi ndio zitakua utambulisho wako kwa blog yako.
Ikishafunguka hiyo inamaana umesha tengeneza akaunti yako ya blogger. Baada ya hapo

03. Chagua aina ya wasifu unaotaka kutumika au kuonekana Na wasomaji katika blog yako, Na baada ya hapo save. Kisha bofya sehemu iliyoandikwa tengeneza blogu (create blog).


04. a. Andika Jina la Blog kwa Herufi KUBWA 
    b. Jina Blog Address kwa Herufi ndogo.
    c & d. Kisha Bonyeza Check Availability ikionesha Sorry, this blog is not available basi jaribu jina lingine mpak ioneshe kijani yaani This blog address is available.
  e.Jaza hayo maneno hapo ili kiunesha kua sio robot bali ni mtu
  f.The bonyeza continue hapo chini kulia kisha kuendelea
05. Baada ya hapo utakua tayari umeshatengeneza Blog yako…unaweza kubonyeza New Post ili kuweka habari au picha, au ukabonyeza View Blog ili kujua muonekano wa blog yako.
06. Sasa waweza kupost Na kualika watu kuanzia kutembelea blogu yako.

*TAHADHARI:
Tengeneza blogu kwaajili ya manufaa Na Sio kwaajili ya mambo yasiyokuwa ya kimsingi.


Kwa yeyote mwenye swali, maoni au ushauri tuandikie hapo chini, laki ni pia kama umekwama au unahitaji blogu Na hujui cha kufanya tuandikie pia.
Asanteni.

Usikose makala ijayo itakayo husu namna ya kutengeneza pesa kupitia blogu yako

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !