Application 5 bora zisizokuwepo Play store.



                                         GET OUR APPLICATION


U hali gani ndugu mpendwa. Baada ya makala yetu iliyopita iliyokuwa ikiangazia mitandao mbalimbali itakayokuwezesha kutengeneza application kiurahisi leo tena tunakuja na application 5 bora zisizokuwepo play store.

Bila shaka wengi wetu tumekuwaa na mazoea ya kuwa Application bora na salama hupatikana kwenye Play store pekee lakini je unajua ya kuwa kuna application bora na salama zaidi ambazo hazipo play store? Huku nyingi zikitolewa na nyingine kukataliwa kabisa kuwekwa Play store.

''Najua swali unalojiuliza na ambalo ungependa kupata majibu ni kwamba ni kwanini application nyingine zitolewe na  nyingine kukataliwa akati ni bora na salama?''
Jibu kwa swali lako ni kama ifuatavyo, Application nyingi zinazo katiliwa au kunyimwa kibali cha kuwekwa Play store ni kwamba zimekuwa zinarahisisha na kutoa huduma zaidi ya kile mtumiaji anachotoa. Inamaana huduma ni ya hali ya juu sana.

Application tunazoenda kuzitoa ni zile tulizo zifanyia uchunguzi wa kina na pia kuzijaribu katika nyakati na vifaa mbali mbali. na baada ya hapo tulikuja na majibu ya fuatayo (kumbuka application tajwa hapo chini haziko kwenye mpangilio wowote, waweza kuzipanga kulingana na mtizamo wako)


1. ShowBox
Hii ni moja kati ya application ambayo sio ngeni masikioni kwa wengi, kutokana hapo mwanzo kuwepo play store lakini baadae kuondolewa.
"Je Showbox hufanya nini?"
Application hii hukupa fursa wewe kuweza kutaza video mpya mbalimbali bila gharama yoyote ina maana ni bure kabisa. Baada ya application hii kutolewa Play store kumekuwa na application mbalimbali na nyingi zilizokuja kwa jina hili lakini ukweli ni kwamba application halisi (original) haipo kwenye soko hilo.

 2. Mobdro
Kati ya application zilizo nyimwa kibali cha kuziwezeshwa kuwekwa play store hii ni moja wapo. Application hii ni moja kati ya application bora na salama sana kwaajili simu na kumpyuta.

"Je Mobdro ina faida gani?"
Hii ni Application itakayo kuwezesha kuangalia TV aina mbalimbali mtandaoni bure bila hata kujisajili au kufungua akaunti. Lakini pamoja na hayo yote ni Application yenye ujazo mdogo sana ukilinganisha na uhondo inayotoa.

3. Tubemate
Kama unakumbuka hapo nyuma application hii ilikuwepo play store na wakati huo youtube ilikuwa haijashika kasi. Lakini baadae application hii iliondolewa play store! Unaweza ukajiuliza ni kwanini basi ilitolewa au ni kwa sababu ni ya zamani?

"Je Tubemate ina uwezo gani kuishinda youtube?"
Ukweli mkubwa ulifichika kwa application hii ni kuwa inakupa uwezo wa kupakua video yoyote direct kutoka youtube na hauhitaji kuwa na application ya youtube (iliyopo play store).  Tumekuwa tukifumbwa macho tukidanganywa kuwa application ya youtube iliyopo play store ndo toleo jipya na ndo inayotambulika lakini si kweli kuna siri nzito nyuma ya pazia (nisingependa kuiongelea sana) jiulize kwanini tubemate iliondolewa play store lakini bado ipo (unknown sources) na inafanya kazi kama kweli ni ya zamani?

4. OGInsta+
Asilimia kubwa ya watanzania tunauelewa na kuutumia mtandao wa kijamii wa Instagram, na hii ni application mojawapoinayomilikiwa na mtandao huo. Application hii haijafanikiwa kuwekwa play store kutokana na uwezo wake.

"Kuna utofauti gani kati ya application hii na Instagram iliyozoeleka(iliyopo play store)?"
Ni mara ngapi umeingia katika akaunti yako ya Instagram(kwenye application ya kawaida) na ukakutana na video au picha uliyoipenda na ungependa kuipakua na kuihifadhi kwenye kifaa chako lakini ukalazimishwa kupakua application ya video "downloader for instagram"? Lakini pia ni mara ngapi umejaribu kukuza (zoom) picha lakini ukalazimika kupakua application ya "Insta zoom"?
Najua ni mara nyingi sana na kwa wengi. Lakini kuwa mjanja kupitia application hii utaweza kufanya hayo yote, na pia application hii cha kushangaza ni ndogo sana.

5. Aptoide_lite
Moja kati ya application ambazo zimerahisisha maisha ya wengi ni hii. Kama unakumbuka Aptoide hapo mwanzo ilikuwa inapatikana play store lakini miaka ya hivi karibuni iliondolewa. Baada ya kuondolewa play store watengenezaji wa Aptoide walitengenezea Aptoidelite.

"Ni kwanini play store waliwatimua Aptoide? lakini Je Aptoidelite ina utofauti gani na Aptoide ya mwanzo?"
Kwanza kabisa Aptoide ni soko la application kama ilivyo play store, lakini utofauti ulionekana pale ambapo Aptoide walikuwa wakitoa au kuwaruhusu watumiaji waki kupakua application nyingi bure mpaka zile zilizo kuwa zikiuzwa play store, na hivyo kutishia soko la play store.
Lakini je Aptoide ina utofauti gani na Aptoidelite? Utofauti mkubwa uliopo kati ya application hizi mbili ni kuwa Aptoidelite ni ndogo kuliko Aptoide.
Ni mara ngapi umekuwa ukipoteza MB zako nyingi sana pindi unapo fanya updates za applications za simu yako? Basi kupitia Aptoidelite sahau kupoteza MB zako bure. Kupitia application hii pindi utakapo fanya updates za application zako basi application husika itatumia MB kwaajili yakuongeza kitu kilicho ongezeka kwenye program husika tu! tofauti na play store ambapo utakapo kuwa unafanya updates utatakiwa kupakua application upya kabisa hivyo kukufanya upoteza MB nyingi sana.

Tafadhari usisahau kutuandikia kama una ushauri, maoni, swali au hata kama unahitaji msaada wowote wa kiteknolojia, lakini pia endelea kutembelea Magoiga2016 kwaajili ya habari na kujifunza maujuzi zaidi ya teknolojia.

Comments :

  1. GBWhatsapp apk Download Latest Version 2018. Download Latest GB Whatsapp for Use 2 Whatsapp in One Mobile.  GBWhatsApp

    ReplyDelete
  2. Your article is extraordinarily smart.I love to browse your diary's posts everyday and that i got vast facilitate from your blog and developed a replacement app mytwc login
    you'll check.Thanks for wonderful diary.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Congrats for the wonderful work and thanks

      Delete

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !