Airtel, Tigo na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na EzyPesa wamefanya zoezi la kutuma na kupokea pesa kwenye huduma zao kuwa rafiki zaidi kwa watumiaji wao. Kuanzia sasa mtumaji pesa kutoka kwenye mitandao hiyo kwenda huduma nyingine katika mitandao hiyo atakatwa gharama ya kutuma ile ile kama anayokatwa akiwa anamtumia mteja wa mtandao kama wake.
Yaani kama mtu anatuma pesa kutoka Airtel Money kwenda Tigo Pesa basi atakatwa gharama za kutuma kama zile ambazo huwa anakatwa akituma kwenda huduma ya Airtel Money.
Kwa kiasi kikubwa uamuzi huu utawasaidia sana wateja wao hasa hasa kwa wakati huu ambao mteja wa mtandao wowote anaweza kuhama mtandao wa simu kwa urahisi zaidi. Jambo hili linafanya uamuzi wa kuhama uwe rahisi kwa watu ambao huwa wanategemea sana huduma za kutuma na kupokea pesa.
Airtel, Tigo na Zantel wamejiunga katika kusambaza elimu kwa wateja juu ya huduma hii kupitia kampeni ya Taifa Moja ambayo tayari inafanyika katika mikoa mbalimbali. Kampeni hiyo imedhaminiwa na taasisi tanzu ya Benki ya Dunia, IFC.
Vipi je wewe ni mteja kati ya huduma hizi? Una maoni gani juu ya hili?

Comments :
Post a Comment
write to us your views on this