Hii ndio simu mpya ya BlackBerry

 Kama wewe ni mpenzi wa simu za blackberry lazima utakua ulikua unajua kwa Blackberry kwa kushirikiana na TLC walifanya uzinduzi wa simu yake mpya ya Blackberry KeyOne, simu hiyo iliyozinduliwa jana huko nchini Barcelona ni moja kati ya simu mpya za mwaka huu zenye kutumia Android kutoka kwa kampuni hiyo ya muda mrefu.
 Sifa za BlackBerry KeyOne
BlackBerry KeyOne inakuja na uwezo mkubwa wa processor kwani inatumia processor ya snapdragon 2GHz octa-core pamoja na RAM ya GB 3 uku ikiendeshwa na mfumo wa uendeshaji wa Android 7.1 Nougat. Kwa upande wa kioo simu hii inatumia kioo cha inch 4.5 kikiwa na resolution ya 1620×1080 pixels pamoja na ukubwa wa memory ya ndani wa GB 32, kwa upande wa kamera simu hii inatumia kamera ya nyuma yenye Megapixel 12 na ya mbele yenye Megapixel 8 Simu hii inaendeshwa na batter yenye nguvu ya 3505mAh ikiwa na uwezo wa kudumu na chaji karibia siku nzima.


Kingine simu hii inawezesha Touch Screen pamoja na Fingerprint zote zikiwa zinapatikana juu ya keyboard ya simu hiyo, kifupi ni kwamba unaweza kugusa kioo au kutumia keyboard au unaweza kugusa keyboard kama sehemu ya Touchscreen. Simu hii inategemea kuingia sokoni hivi karibuni kwa dollar za marekani $549 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 1,300,000.

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !