Kuna njia mbalimbali za kufufua flash iliyokufa, njia hizi zifuatazo zimegawanyika kwa makundi makuu matatu kila kundi lina hatua zake, hivyo chagua njia mbayo itakua rahisi kwako kisha fuata hatua zake. Nauhakika ukifuata kwa ukamilifu njia hizi na hatua zake lazima utaweza kufufua flash yako iliyokufa kwa urahisi kabisa.
01. Badilisha Jina na Herufi ya Flash
Kila kifaa kinacho chomekwa kwenye kompyuta huonekana kwa jina na herufi kwa mbele, kwa kubadilisha jina na herufi ya flash yako unaweza kufanya flash yako kufanya kazi tena na kuanza kuonekana tena kama awali (kumbuka unaweza kufanya hatua hii pale flash yako inapoonekana lakini huwezi kuifungua)
Hatua
Chomeka flash kwenye kompyuta yako nenda kwenye icon iliyoandikwa My Computer kisha bofya kibonyezo cha kulia kwenye mouse yako kisha chagua Manage. Baada ya hapo chagua Disk Management iliyoko upande wa kushoto chini kidogo. Chagua flash au memory unayotaka kurekebisha au kufufua, kisha bofya kibonyezo cha kulia kwenye mouse yako na chagua “Change Drive Letters and Paths.”
Baada ya hapo chagua herufi kwenye list inayoonekana upande wa kulia, hakikisha unachagua herufi ambayo haitumiki au haijatumika kwenye kompyuta yako. Baada ya hapo bofya ok kisha hapo hapo utaona flash yako imerudi kuonekana kama kawaida.
02. Install Tena Driver za Flash Yako
Kuna wakati flash yako inashindwa kuonekana kwenye kompyuta yako kutokana na kompyuta yako kushindwa kugundua driver za flash yako, hivyo kwa kutumia njia hii utaweza kuondoa driver zilizopo kwenye kompyuta yako na kuzirudisha tena ili kuwezesha kompyuta yako kugundua driver hizo ili flash yako iweze kuonekana.
Hatua
Chomeka flash kwenye kompyuta yako nenda kwenye icon iliyoandikwa My Computer kisha bofya kibonyezo cha kulia kwenye mouse yako kisha chagua Manage. Baada ya hapo chagua “Device Manager” iliyoko upande wa kushoto chini kidogo. Baada ya hapo chagua “Disk Drives” iliyoko juu kabisa na utachagua jina la flash yako kisha bofya na bonyeza “Uninstall” kisha bofya OK. Baada ya hapo chomoa flash yako kisha restart kompyuta yako na ikisha waka tena chomeka flash yako na acha kwa muda kama dakika moja au zaidi baada ya kuchomeka flash yako, acha imalize kuinstall driver zote kisha utaona flash yako ikifunguka.
03. Format Flash kwa Kutumia CMD au Command Prompt
Njia hii ni moja kati ya njia mbazo zinaitaji umakini sana kwani ni njia mbayo inachanganya kidogo lakini njia hii imeonekana kusaidia watu wengi sana na inaonekana kufanya kazi kwa kiwango kikubwa kuliko njia nyingine.
Hatua
Chomeka flash yako au Hard Disk kwenye kompyuta yako na hakikisha hakuna kifaa kingine chochote kilicho chomekwa kwenye kompyuta yako zaidi ya kifaa hicho. Washa programu ya CMD au Command Prompt kwenye kompyuta yako, baada ya kuwasha programu hiyo andika diskpart kisha bofya Enter ikiuliza ruhusa bofya Ok na endelea na hatua zinazofuata.
Andika list disk kisha bofya Enter na hapo utaweza kuona vifaa vyako vyote ambavyo umevichomeka kwenye kompyuta ikwepo flash au hard disk ambayo unataka kuifufua, baada ya hapo kwa umakini angalia namba ya disk ambayo unataka kufufua kisha andika select disk kisha andika namba ya disk kwa mbele ya maneno hayo kisha bofya Enter.
Baada ya hapo andika Clean kisha bofya Enter na kisha andika create partition primary na baada ya hapo andika active na bofya Enter, baada ya hapo andika select partition 1 kisha bofya Enter alafu baada ya hapo andika format fs=fat32 kisha bofya Enter, Baada ya kufuata hatua zote hizo hapo juu kwa uhakika subiri kwa muda kidogo na pale itakapo maliza kuformat flash yako itakuwa iko tayari kwa kutumia na nauhakika itakuwa imefufuka kabisa.
Comments :
Post a Comment
write to us your views on this