Facebook na Apple pia kumpinga Rais Trump.



Sakata zima la maswala ya uhamiaji nchini marekani linaendela wakati huu makampuni takriban 97 ya teknolojia ya nchini marekani yameamua kuungana na kupinga swala zima la raisi huyo kupinga waamiaji kutoka nchi mbalimbali.

Makampuni hayo yamefungua mashtaka kwenye mahakama ya Washington state court ili kupinga ubaguzi huo wa waamiaji kutoka nchi mbalimbali ambazo zilitajwa na rahisi huyo mapema wiki mbili zilizopita. Katika kufanya hivyo makampuni hayo yalituma Amicus briefs kwenda kwa mahakama hiyo ikitaka mahakama kufikiria shauri hilo la kuzuiwa kwa waamiaji kutoka nchi za kislamu zilizotajwa na raisi huyo.

Makampuni hayo yalio tuma nyaraka hiyo mahakamani ni pamoja na Apple, Facebook, Google, Twitter, pamoja na Microsoft, kama unataka list nzima ya makampuni hayo unaweza kudownload nakala ya nyaraka hiyo yenye ripoti hiyo pamoja na majina yote ya makampuni yanayo mpinga raisi donald trump kwenye swala hilo.


Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !