Kampuni ya utengenezaji kompyuta kwa ajili ya matumizi ya uchezaji magemu, Razer, watambulisha laptop yenye vioo vitatu (display) kwa wakati mmoja.
Laptop hiyo ambayo kwa sisi
inafahamika kwa jina la kimatengenezo zaidi, Project Valerie,
imetambulishwa kwenye maonesho ya bidhaa za elektroniki huko jijini Las
Vegas nchini Marekani.
Laptop hii inakuwa ya kwanza duniani kuja na mfumo huu.

Kikawaida inaonekana kama laptop ya
kawaida ila kwenye kioo kioo kikuu vingine viwili vinavyochomoka upande
wa kulia na kushoto na kujipanga.
Kilaa screen/display/kioo
kimoja kina ukubwa wa inchi 17, takribani sentimenta 43. Display zake ni
za kiwango cha juu cha HD, 4K.

Uwepo wa screen tatu kunaweza mfanya
mtu afikiri laptop hiyo itakuwa nene sana pale itakapofunikwa, ila
wamejitahidi kuifanya isiwe nene sana. Ina unene wa inchi 1.5, takribani sentimita 3.81.
Kampuni ya Razer bado hawajatoa muda
rasmi ambao laptop hizo zitaingia sokoni ila lazima bei yake itakuwa juu
kidogo ila inategemewa kwa wapenzi wa magemu ambao tayari wamezoea
kutumia display zaidi ya moja katika uchezaji wa magemu kwenye kompyuta
watakuwa tayari kujitoa na kununua laptop hii.
Comments :
Post a Comment
write to us your views on this