Mwaka mmoja wa kuwa hewani.

U hali gani msomaji mpendwa wa Magoiga2016. Bila shaka hujambo na heri ya Christmas.
Ikiwa ni tarehe 25/12/2017, tungependa kukuletea historia fupi ya tovuti hii ikiwa inatimiza mwaka mmoja.
Magoiga2016.blogspot.com ni tovuti ndogo (blogu) inayotoa habari za kiteknolojia kwa lugha za kiswahili na kiingeleza.



*KUANZISHWA KWAKE*
Magoiga2016 ilianzishwa mnamo mwaka 2014 ikiwa chini ya umiliki wa Magoiga. Magoiga alianzisha blogu hii akiwa kidato cha tatu (3) katika shule ya sekondari ya ufundi Ifunda iliyopo mkoani Iringa.
Mwaka 2014 mpaka mwaka 2016 blog hii haikuweza kufanya vizuri, na hii ni kutokana na mmiliki (Magoiga) kukosa, mda na vitendea kazi vya kutosha, kufikia mwaka 2016 Magoiga aliamua kuifufua upya blog hii na mpaka leo ipo hewani.

 Magoiga Mtatiro (mmiliki)

"Kabla hata ya kuanzisha blog hii alikuwa akisema kwa wenzake tulikuwa tukiongea kiutani nae na alipenda sana kusema atakuja kumiliki tovuti au blog, lakini sisi tulichukulia utani" Anasema Jackson Lazaro.

"Nilikuwa nikiwambia wenzangu kuhusu kumiliki blog lakini ni wachache sana walioniamini, wengi wao walichukulia kuwa mzaha na maasiala mengi! Lakini sikukata tamaa" Anasema Magoiga.
Soma chapisho la kwanza, la 25/12/2016

*MAFANIKIO*
Katika kila jambo tunalofanya au kuanzisha huwa tunakuwa tunataka faida au mafanikio.
"Wakati naanzisha blog hii sikuwa na malengo ya kupata pesa. Lengo langu kubwa lilikuwa kuwa na uwezo wa kusambaza habri za kiteknolojia" Anasema Magoiga.
Mafanikio makubwa Magoiga aliyoyapata kupitia blog hii ni kama ifuatavyo;
(i) Takribani watembeleaji (views) 3,500 kwa mwezi
(ii) Takribani wafuatiliaji wa karibu (subscribers) 10,000. kwa kipindi cha mwaka mmoja.
(iii) Kutengeneza na kuwashilikisha vijana katika fursa mbalimbali (Ajira). Tumefanikiwa kuajili vijana 10 ndani ya mwaka mmoja.

"Mimi kama mtumiaji wa mtandao, huwa sipendi kuona matangazo pindi ninapokuwa natumia mtandao, ndo maana sipendi kuweka matangazo kwenye blog yangu" Anasema Magoiga.

*WASHIRIKA WETU WAKUU*
Magoiga2016 imekuwa ikishirikiana na mashilika, makampuni na watu binafsi mbalimbali. Hii yote ni kwaajili ya kuwezesha ufikishaji wa habari kwa watu wengi zaidi.
Kampuni kuu ambayo Magoiga pia mmoja wa waendeshaji (akiwa ni PROGRAMMER) wa Project-X



Kampuni hii pia ilianzishwa na Magoiga ambae ni mmiliki wa blog hii. Nia na madhumuni ikiwa ni kuweza kusaidia jamii kuweza kukua kiteknolojia.
washirika wengine wa kampuni hii ni pamoja;
Mica herma mrema (mmiliki wa blog ya Gaming City )
akiwa na kazi kuu ya kutoa ushauli juu ya kazi mbalimbali.
Sylvester Johnbosco. akiwa kama marketing manager wa kampuni.
 PROJECT-X 👽 clue
*NENO LA SHUKRANI*
"Binafsi ningependa kuwashukuru wale wote waliofanikisha ndoto yangu kutimia, ni wengi sana kiasi kwamba sina hata uwezo wa kuwataja wote, lakini kwa niaba ningependa kumshukuru kaka yangu Simon Ernest ambae amekuwa bega kwa bega nami kafika kufikia ndoto zangu, wasomaji wangu wote wa magoiga2016 asanteni sana" Anasema Magoiga

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !