Ifahamu Programu wezeshaji inayoweza kujua unachofikiria!

Wanasayansi wamekuwa wakivumbua vitu kila leo. Tukianzia kwenye roboti, drones, gari zinazojiendesha zenyewe, n.k. Wanasayansi wameweza kutengeneza programu wezeshaji unayoweza kujua unafikiria nini.


Timu ya watafiti imeweza kutengeneza programu wezeshaji (software) yenye uwezo wa kutafasiri data kutoka kwenye MRI na kutengeneza picha halisi ya mtu aliyekuwa mgonjwa alipokwa kwenye mashine hiyo.

Huko nyuma programu wezeshi (software) iliweza kutoa majibu ingawa picha zilizokuwa hazionekani vizuri (zilionekana kwa rangi nyeupe na nyeusi) yaani kama picha zilizokuwa zikipigwa miaka ya 70 kurudi nyuma.
Programu hiyo endeshaji itasaidia sana kuweza kujua ni jinsi gani ubongo unavyofanya kazi kwani mashine hii inaweza kujua unachokifikiria na sio kwa kubahatisha bali kwa uhakika na kutoa majibu yaliyosahihi.

Je, unadhani teknolojia hii ikifika kwetu Afrika itakuwa na faida/madhara gani kwetu? Toa maoni yako hapo chini nipate kusikia kutoka kwako msomaji wetu.

Comments :

  1. Hello,
    The program name has not been released yet

    ReplyDelete

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !