Mpango wa Uchina kupeleka binadamu kuishi kwenye mwezi

 ambo la kufanya tafiti za anga kwa nchi kama Uchina, Marekani, Urusi na hata India limekuwa jambo ambalo si la kustaajabu tena kwani tafiti hizo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara na hata roketi kurudi salama.


Nchi ya Uchina imedhamiria kwetu hatua zaidi katika masuala ya tafiti katika masuala ya anga na sasa imeanza kufanyia majaribio mpango wa kupeleka binadamu wakaishi kwa muda mrefu kwenye Mwezi.

 china kupeleka binadamu mwezini: Suala la teknolojia ya anga za juu limekuwa ni la ushindani kwa mataifa makubwa na sasa China pia wanataka kuonesha ubabe
Mpango kazi ukoje?

Jumatano ya Juni 10 Wanafunzi wanne wa taaluma ya anga za juu wanaosomea shahada za juu chuo kikuu cha Beihang walihamia chumba hicho maalum, ambacho kimepewa jina Yuegong-1 likiwa na maana ya jina hilo ni Kasri la Mwezi.

Watakaa katika chumba hicho maalum kwa siku 60, lakini watafuatiwa na kundi jingine la wataalamu ambao watakaa kwa siku 200 mfululizo. Wanne hao kisha watarejea na kukaa kwa siku 105.
 aisha ya angani yatakuaje?

Mpango wa kutuma watu wakakae muda mrefu kwenye Mwezi utajumuisha kutumwa kwa sehemu mbili kubwa za mtambo za kukuzia mimea, na sehemu nyingine kubwa sawa na nyumba ambao itakuwa na vyumba vinne vya kulala, sebule moja, bafu, chumba cha kubadilishia taka na chumba cha kufugia wanyama.

Kinyesi cha binadamu kitaozeshwa kwa kutumia viumbe hai. Mimea na mboga itakuzwa kwa kutumia taka mbalimbali za chakula na matumizi mengine.

Lengo ni kuwaanda kwa safari ya kuishi kwa muda mrefu kwenye kituo cha anga za juu kwenye Mwezi, bila kupokea usaidizi wowote kutoka ardhini lakini Uchina haijapanga kutuma wana anga wengine kwenye Mwezi kabla ya miaka 10 kupita.

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !