Laptop bora kwaajili ya kuchezea magemu

Linapokuja swala zima la laptop bora ukweli ni kwamba kila mtu anajua kile kilicho bora kwake kutokana na matumizi ya laptop au kompyuta hiyo, sababu hiyo ndio haswaa iliyo sababisha leo Magoiga2016 kukuletea list ya laptop bora kwaajili ya game kwa mwaka huu wa 2017.

01. Asus ROG Strix GL502

Asus ROG Strix GL502 ni moja kati ya laptop ambayo ni bora sana tena sana kwako wewe mpenzi game kwani sifa pamoja na graphics za laptop hii hakika zina uwezo wa kuimili game yoyote ya kwenye kompyuta.

Sifa za Asus ROG Strix GL502

CPU: Intel Core i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 – 1070
RAM: 16GB DDR4
Screen: 15.6-inch full HD 1,920 x 1,080 IPS
Storage: 128GB – 256GB SSD, 1TB HDD

02. Alienware 13 R3

Kuna laptop chache sana za game zenye uwezo wa Alienware 13 R3, laptop hii inauwezo mkubwa pamoja na kioo chenye teknolojia bora ya OLED. Hivyo kama unaitaji kompyuta bora ya kucheza game basi laptop hii ni bora sana kwako.

Sifa za Alienware 13 R3

CPU: Intel Core i5 – i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060
RAM: 8GB – 16GB DDR4
Screen: 13.3-inch HD 1,366 x 768 TN – QHD 2,560 x 1440 OLED touchscreen
Storage: 180GB – 512GB SSD

03. HP Omen 17

Laptop hii ni moja kati ya laptop bora na nzuri sana pia kama wewe ni mpenzi wa laptop zenye uzito kiasi HP Omen 17 ni laptop bora kwako, vile vile kizuri zaidi kuhusu laptop hii ni kioo chake kwani kinauwezo wa 1440p hii ni sawa na kusema laptop hii ina teknolojia ya 4K.

Sifa za HP Omen 17

CPU: 6th gen Intel Core i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1070 (8GB GDDR5);
Intel HD Graphics 530
RAM: 16GB DDR4
Screen: 17.3-inch 4K (3,840 x 2,160) IPS with G-Sync
Storage: 1TB – 2TB HDD, 128GB SSD

04. Gigabyte Aero 14

Laptop hii ni moja kati ya laptop ambazo ni bora sana hasa kama unapenda laptop ambazo ni ndogo na zenye nguvu kubwa. Pia laptop hii ya Gigabyte Aero 14 ni moja kati ya laptop zenye bai nafuu sana kwenye masoko mbalimbali ya mitandaoni, ukilinganisha na laptop nyingine kwenye list hii.

Sifa za Gigabyte Aero 14

CPU: Intel Core i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 (6GB GDDR5)
RAM: 16GB – 32GB
Screen: 14-inch, QHD 2,560 x 1,440 anti-glare IPS
Storage: 512GB – 1TB SSD

05. Razer Blade

Kwa wacheza game wengi laptop hii ni bora sana kwani inauwezo bora sana pamoja na kuchangiwa na uwezo wake wa kudumu na battery kwa masaa 3 na dakika 35 ukiwa unacheza game na masaa 6 kama una angalia video bila kupumzika. Kwa hakika Razer Blade ni moja kati ya laptop bora sana za game kwa mwaka huu 2017.

Sifa za Razer Blade

CPU: 2.6GHz Intel Core i7-6700HQ
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 (6GB GDDR5 VRAM)
RAM: 16GB
Screen: 14-inch FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800) IGZO (LED backlit, multi-touch)
Storage: 256GB – 1TB PCIe SSD

06. Aorus X5 v6

Unaweza ukawa huijui sana laptop Aorus X5 v6 lakini hii ni moja kati ya laprop bora sana za game kwa mwaka huu, unaweza kutuia kompyuta hii kucheza game za aina yoyote ile ziwe zenye teknolojia ya HD.

Sifa za Aorus X5 v6

CPU: Intel Core i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1070 (8GB GDDR5)
RAM: 8GB – 16GB
Screen: 15.6-inch, FHD 1,920 x 1,080 – WQHD+ 2,880 x 1,620 IPS
Storage: 1TB HDD; 256GB SSD

07. Razer Blade Pro

Kama unatafuta laptop bora ya kucheza game yenye kioo cha inch 17 pamoja na teknolojia ya 4K basi Razer Blade Pro ni laptop bora sana kwako. Laptop hii ni moja kati ya laptop zilizongelewa sana kwa mwaka 2016 lakini pia mwaka huu bado laptop hii ni laptop bora sana kwa wapenda game kote duniani.

Sifa za Razer Blade Pro

CPU: Intel Core i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1080 (8GB GDDR5)
RAM: 32GB
Screen: 17.3-inch, UHD (3,840 x 2,160) IGZO touchscreen with G-Sync
Storage: 512GB – 2TB PCIe SSD

08. Origin EON17-X

Hii ni laptop nyingine ambayo kwa hakika ni moja kati ya laptop bora sana za kucheza game kwa sasa, laptop hii ina kioo chenye teknolojia ya 4K hivyo jiandae kucheza game zenye muonekano angavu pale unapokua na Laptop hii ya Origin EON17-X.

Sifa za Origin EON17-X

CPU: Intel Core i5 – i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 1060 – 1080
RAM: 8GB – 64GB
Screen: 17.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QFHD (3,840 x 2,160) Matte Display with G-Sync
Storage: 120GB – 2TB SSD, 500GB – 2TB HDD, 1TB – 2TB SSHD

09. Acer Predator 17 X

Namba 9 kwenye list hii ni Acer Predator 17 X, laptop hii ni moja kati ya laptop za kisasa kabisa zenye uwezo wa kucheza game zenye kuitaji graphics card ya aina yoyote. Laptop hii ina tumia feni zenye teknolojia ya kisasa ili kufanya laptop yako kukaa kwa muda mrefu ikiwa imepoa. Hivyo laptop hii ni moja kati ya laptob bora ukizingatia laptop hii ni maalum kwa kucheza game.

Sifa za Acer Predator 17 X

CPU: Intel Core i7
Graphics: Nvidia GeForce GTX 980
RAM: 32GB DDR4
Storage: 1TB HDD, 512GB SSD

10. Origin EON17-SLX

Laptop ya mwisho ya kweli list hii ni Origin EON17-SLX laptop hii ni moja kati ya laptop za kisasa na zenye uwezo mkubwa hasa pale linapokuja swala zima la game. Laptop hii yenye inch 17 ni moja kati ya laptop ya yenye uwezo mkubwa sana.

Sifa za Origin EON17-SLX

CPU: Intel Core i5 – i7 |
Graphics: NVIDIA GeForce GTX 1070 – 1080 |
RAM: 8GB – 64GB |
Screen: 17.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – UHD (3840 x 2160) IPS Matte Display with G-SYNC
Storage: 120GB – 4TB SSD, 500GB – 1TB HDD, 1TB SSHD


Na hizo ndio laptop bora kwaajili ya wapenda game wote kwa mwaka huu 2017, kama una maoni ushauri au hata kama unadhani kuna laptop tumeisahau tuandikie hapo chini ili tuweze kuiongeza kwenye list hii.

Comments :

Post a Comment

write to us your views on this

Interested to get more of our Update !